Viongozi wa makanisa eneo la Malindi kaunti ya Kilifi, sasa wanataka viongozi wa kisiasa kusalia ndani ya vyama vyao na wala sio kukiuka misingi ya vyama na kusababsisha malumbano.
Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Makanisa katika kaunti ya Kilifi Askofu Thomas Kakala, viongozi hao wametaka wanansiasa kuzinagtia kanuni za vyama vya kisiasa badala ya kuonekana kukosa udhabiti.
Askofu Kalala amesema sio vyema kwa viongozi wa kisiasa kutumia mpango wa maridhiano maarufu Handshake na kukosa misimamo wa kisiasa.
Wakati uo huo amewataka wakaazi wa maeneo bunge ambapo huenda kukafanyika uchaguzi mdogo hasa eneo bunge la Malindi na Msambweni kuhakikisha wanawachugua viongozi wenye nidhamu na wawajibikaji.
Taarifa na Charo Banda.