Kampuni zinazojishughulisha na uchimbaji madini katika Kaunti ya Kwale zimehimizwa kuzingatia maslahi na haki za Wakaazi.
Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu nchini Haki Afrika limedaiwa kwamba kampuni hizo zimewabagua Wakaazi licha kwamba zinahitajika kutekeleza majukumu yao kuinufaisha jamii.
Akizungumza katika afisi za Shirika hilo Mjini Mombasa, Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Hussein Khalid ameitaka Serikali ya Kaunti ya Kwale na ile kuu kuhakikisha kwamba kampuni hizo zinatekeleza majukumu yake kuambatana na sheria za madini nchini na zaidi kwa kuzingatia haki za kibinadamu.
Khalid amesema kuwa wakaazi wanaoishi pambizoni mwa kampuni hizo wamelalamikia kuathirika kiafya huku wakikosa kunufaika na ajira.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.