Story by: Our Correspondents
Kampuni ya usambazaji maji katika kaunti ya Taita taveta ya TAVEVO imewataka wakaazi wa kaunti hiyo kuwasilisha ripoti kwa kampuni hiyo, pindi wanaposhuhudia changamoto za aina yoyote katika mita za maji.
Afisa mkuu wa masuala ya kiufundi katika kampuni hiyo Livingston Righa amesema kwa sasa wanatumia mita za kisasa na zinaweza kukaguliwa vyema na kampuni hiyo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni hiyo Richard Kibengo amesema wanaendeleza mikakati ya kuhakikisha kampuni hiyo inatoa huduma zake kwa njia ya kidijitali.