Kampuni ya uchimbaji madini ya Base Titanium, imewahakikishia wakaazi wanaoishi kwenye maeneo ambayo kampuni hiyo inanuia kuchimba madini kuwa watafidiwa.
Afisa msimamizi wa miradi ya jamii katika kampuni hiyo Juma Lumumba amesema kuwa zoezi la kupanua uchimbaji madini litaanza na utafiti wa kubaini sehemu zilizo na madini, kabla ya uchimbaji , huku akiahidi kuwa watakaoathirika watafidiwa kikamilifu.
Lumumba ameongeza kuwa zoezi hilo litafanyika baada ya ushauri wa kina na wakaazi, pamoja na wadau wengine husika ili kuhakikisha kuwa maoni ya kila mmoja yametiliwa maanani.
Wakati uo huo, afisa huyo amekanusha madai ya kudorora kwa uhusiano kati ya kampuni hiyo na wakaazi, akisema kuwa wakaazi wa Kwale wananufaika pakubwa kutokana na shughuli za kampuni hiyo.
Taarifa na Michael Otieno.