Kampuni ya uchimbaji madini Base titanium imetoa ufadhili wa chakula pamoja na vifaa vya afya vya kujikinga na maambukizi ya Corona kwa Serikali ya Kaunti ya Kwale.
Afisa wa uhusiano mwema katika kampuni hiyo Pius Kassim amesema chakula hicho ambacho ni magunia ya mchele , maharagwe mahindi uto na vifaa vya afya vimegharimu shilingi milioni sita.
Akitoa bidhaa hizo kwa Kaunti Kassim amesema wametoa pia mitungi sitini ya vieuzi / sanitizers na matangi ya maji ambayo wataeka katika vijiji 40 ili kuwezesha wakazi kuosha mikono.
Kassim amesema kampuni hiyo itashrikiana na serikali ya kaunti ya Kwale kuhakikisha wanasaidia wakwale kujikinga kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona.
Kwa upande wake gavana wa kaunti ya Kwale Salim Mvurya amepongeza hatua hiyo ya kampuni ya Base Titanium akisema itasaidia kaunti wakati huu wa janga la Corona.