Mbunge wa Rabai William Kamoti ameahidi kukarabatiwa kwa barabara zote katika eneo bunge hilo.
Kamoti, amesema suala la muundo msingi linafaa kushuhukiliwa na viongozi wote sio tu kuachia majukumu baadhi yao, kwani hatua hiyo huenda ikazidi kurudisha nyuma masuala ya maendeleo.
Akizungumza na wanahabari, Kamoti amesema tayari mikakati ya kukarabati barabara ya Kombeni- Jimba- Mtandikeni katika eneo bunge hilo pamoja na daraja dogo eneo hilo imeanza kushuhulikiwa.
Kamoti amewataka wakaazi kuwa waangalifu zaidi pindi wanapowachagua viongozi wakati wa uchaguzi, akidai kuwa baadhi yao hawajali matakwa ya wananchi wao.
Taarifa na Mercy Tumaini.