Picha kwa hisani –
Kamishna wa kaunti ya Kilifi Kutswa Olaka amewataka wahudumu wa magari ya uchukuzi wa umma kuzingatia sheria za Covid-19 ili kuwakinga abiria dhidi ya maambukizi ya Corona.
Akizungumza hapo jana, Olaka amesema kuanzia tarehe 22 mwezi huu wa disemba,yaani hii leo ni lazima magari yote ya uchukuzi wa umma katika kaunti ya Kilifi yawe na cheti maalum cha kujikinga na Corona.
Kwa upande wao madereva wa magari ya uchukuzi wa umma katika kaunti hiyo Wamesema imekuwa changamoto kupata cheti hicho kutokana na ukosefu wa fedha.