Katibu katika Wizara ya usalama wa ndani Dkt Karanja Kibicho, ametangaza mabadiliko kadhaa yaliyofanywa na Wizara hiyo katika ngazi ya makamishna wa kaunti.
Katika mabadiliko hayo Kamishna wa kaunti ya Kwale Karuku Ngumo amehamishiwa kaunti ya Meru huku nafasi yake ikichukuliwa na Joseph Muriithi aliyekuwa akihudumu katika kaunti ya Busia.
Kamishna wa kaunti ya Garissa Michael Mwangi amehamishwa kaunti ya Homabay huku Joseph Kipkoech akipelekwa kaunti ya Garissa, Abdirizik Jaldesa wa kaunti ya Kisii akihamishwa kaunti ya Samburu.
Hata hivyo wengine waliopewa uhamisho ni manaibu Kamishna ambapo Obel Ojwang amehamishwa eneo la Imenti Kazkazini kutoka eneo la Wajir Kazkazini, Martin Riungu akipekekwa eneo la Nyando, na Elvis Korir akipelekwa eneo la Suba.
Wakati uo huo Kibicho amesema mabadiliko hayo yameanza mara moja huku akisema hatua hiyo ni kuimarisha juhudi zaidi ya kuboresha usalama katika maeneo ya mashinani.