Taarifa na Sammy Kamande.
Mombasa, Kenya, Juni 26 – Kwa mara nyengine tena idara ya usalama kaunti ya Mombasa imejitokeza na kuwasihi wakaazi wa kaunti hiyo kuwafichua walanguzi wa dawa za kulevya.
Kamishna kaunti hio Evans Achoki amesema endapo jamii itakuwa mstari wa mbele katika kufichua walanguzi,visa vya vijana kujiingiza kwenye utumizi wa dawa za kulevya vitapungua.
Achoki amedai kuwa waraibu wa mihadarati wamechangia ongezeko la visa vya utovu wa usalama katika maeneo mbali mbali kaunti ya Mombasa.