Mwenyekiti wa kamati ya bunge la seneti kuhusu uchukuzi na miundo msingi na pia Seneta wa Kiambu Wamatangi kimani amedai kuwepo na haja ya kukarabati na pia kununua feri mpya katika kivuko cha Likoni.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Mombasa baada ya kuzuru kivuko cha Likoni Wamatangi amedai usalama wa mwananchi katika kivuko hicho haujazingatiwa kikamilifu.
Kwa upande wake seneta mteule katika kaunti ya Kilifi Christine Zawadi amelitaka shirika la la Feri kupanga mikakati mbadala ya kurekebisha feri ambazo zinavukisha watu zilizoko katika hali mbaya sawia na kuwaajiri wapiga mbizi ili kuhakikisha wanalinda usalama wa wananchi wanaotumia kivuko hicho kila siku.