Picha Kwa Hisani
Afisa mkuu mtendaji wa mamlaka ya kusambaza dawa na vifaa vya matibabu nchini KEMSA Jonah Manjari na wenzake wawili wanatarajiwa kufika mbele ya kamati ya bunge la seneti huhusu afya kuhojiwa kuhusu sakata ya ufisadi inayowakabili.
Manjari pamoja na Charles Juma aliye mkuu wa kitengo cha ununuzi na Eliud Mureithi mkurugenzi wa biashara katika mamlaka hio wanatuhumiwa kwa kuongeza bei kwa vifaa vya kujikinga na corona vilivyosambazwa katika kaunti za humu nchini na kupelekea ufujaji wa mabilioni ya fedha za kupambana na corona.
Kikao cha kuwahoji watatu hao kilichoandaliwa siku ya ijumaa juma lililopita kilihairishwa na mwenyekiti wa kamati hio seneta Mbito Michael baada ya Manjari kukosa kufika mbele ya kamati hio kwa misingi kwamba alikua mgonjwa.
Watatu hao waliachishwa kazi siku chache zilizopoita ili kutoa nafasi kwa asasi husika za serikali kuendeleza uchunguzi kuhusu sakata hio inayowakabili.