Picha kwa Hisani –
Kamati ya bunge kuhusu usalama wa kitaifa imetamaushwa na mazingira duni ya nyumba za Maafisa wa polisi katika Kaunti ya Mombasa.
Kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Paul Koinange imesema hali hio ni aibu kwa taifa akisema ni sharti mikakati ya dharura iidhinishwe ili kuwaboreshea polisi makaazi yao.
Akizungumza alipozuru nyumba za Maafisa wa polisi za Mbaraki kisiwani Mombasa, Koinange amesema ni kutokana na mazingira duni ndipo polisi wamekuwa wakikabiliwa na msongo wa mawazo na hata wengine kujitoa uhai
Koinange amelitaja swala la marupuru kwa maafisa wa polisi kama litakalotiliwa mkazo na kulishinikiza bunge kulijadili swala la nyongeza ya bajeti ili kuyaboresha mazingira wanayoishi Maafisa wa polisi Pwani na kwingineko nchini.
Kamati hiyo hii leo inazuru Kaunti ya Kwale kukagua makaazi ya Maafisa wa polisi sawa na Kaunti zengine za Ukanda wa Pwani kwa lengo la kutathmini hali halisi ya makaazi ya Maafisa wa polisi.