Taarifa Sammy Kamande.
Kamanda mpya wa polisi kaunti ya Mombasa Augustine Ndhumbi amewataka wakaazi wa kaunti hiyo kushirikiana na idara ya usalama katika kuimarisha usalama wa kaunti hiyo.
Akizungumza kule mjini Mombasa, Ndhumbi amedai kuwa ili usalama uimarishwe zaidi ni lazima wakaazi wawafichue wanaotatiza usalama wa kaunti hiyo.
Kwa upande wake aliyekuwa kamanda wa posili Johnstone Ipara amesema ushirikiano baina ya jamii na maafisa wa usalama umechangia pakubwa katika kuimarisha usalama kaunti ya Mombasa.
Naye aliyekuwa Meya wa Mombasa Ahmed Muhdhar amewahimiza vijana kuwafunzisha vijana wenzao kuhusu umuhimu wa maadili na kujitenga na visa vya utovu wa usalama na itikadi kali.