Picha kwa hisani –
Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amesema uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Msaambweni sio wa mashindano baina ya Naibu rais Dkt William Ruto na Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga.
Akizungumza katika afisi za makao makuu ya Chama hicho kule Nairobi, Kalonzo amesema chama hicho kiko tayari kugeuza wimbi la kisiasa katika uchaguzi huo mdogo ulioratibiwa kufanyika Disemba 15.
Kalonzo amesema chama cha Wiper hakitatikiswa na wafuasi wa chama cha ODM wanaodai kuwa eneo bunge la Msambweni ni ngome ya ODM, akiwaahidi wafuasi wa chama cha Wiper kujitayarisha kwa ushindi wa uchaguzi huo mdogo.
Hata hivyo amezidi kuwarai viongozi wa chama cha Jubilee kuunga mkono mgombea wa kiti hicho kupitia chama cha Wiper kutokana na viongozi wa chama cha Jubilee kutangaza kutoidhinisha mgombea yeyote katika uhaguzi huo.