Picha kwa Hisani –
Kinara wa Chama cha WIPER Kalonzo Musyoka ameweka wazi kuwa atakuwa miongoni mwa wagombea wa kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.
Akizungumza kwenye kikao kilichowaleta pamoja wanachama wa chama hicho, Kalonzo amesema wanaendeleza majadiliano na Katibu mkuu wa WIPER pamoja na viongozi wakuu wa chama hicho kuhusu suala hilo.
Kalonzo amesema baada ya majadiliano hayo, viongozi wote wa chama hicho watakutana ili kupanga mikakati itayowawezesha kujiandaa vyema na kuibuka na ushindi wakati wa kinyang’anyiro hicho.
Akigusia swala la BBI, Kinara huyo wa Wiper amedokeza kuwa ni lazima mchakato wa BBI utiliwe mkazo na ripoti hiyo ipitishwe kwani itabadili mfumo wa uongozi nchini.