Kinara wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amevunja kimya chake na kuweka wazi kuwa atajitosa kikamilifu katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa uraia mwaka wa 2022.
Akiwahutubia wakaazi wa Mombasa baada ya kufungua rasmi afisi ya chama hicho katika eneo bunge la Mvita, Kalonzo ameshikilia kuwa hatawahi kuunga mkono kiongozi yeyote tena katika uchaguzi wa urais ikiwemo Kinara wa ODM Raila Odinga.
Kalonzo amewataka wakaazi wa kaunti ya Mombasa na Pwani kwa jumla kujiandaa kwa uchaguzi mkuu ujao, huku akisema ana imani ya kunyakua kiti cha urais mwaka wa 2022.
Akigusia swala la ukosefu wa ajira kwa vijana, Kalonzo amesema iwapo atashinda uchaguzi huo atahakikisha vijana wananufaika na mpango wa ajira huku akisema atazuru kila eneo la taifa hili kuimarisha umaarufu wa chama hicho.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kitaifa wa Chama cha Wiper Balozi Chirau Ali Mwakwere, amesema chama hicho kimeweka mikakati ya kuhakikisha Vijana Wana nafasi na maamuzi muhimu katika maswala ya uongozi wa nchi.
Hata hivyo katika zaira hiyo yake ya kisiasa kanda ya Pwani, Kalonzo ameandamana na Naibu wake Farah Maalim viongozi mwa viongozi wengine.