Kinara wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amewasihi wakenya kujitenga na siasa za migawanyiko, kidini na kikabila na badala yake kuangazia amani na umoja wa taifa hili.
Akizungumza wakati alipohudhuria ibada ya Jumapili katika Kanisa la Redemed eneo la Ukunda kaunti ya Kwale, Kalonzo amesema bado taifa linakabiliwa na msukosuko wa janga la Corona na ni vyema wakenya washirikiane kuboresha uchumi.
Naye Mwenyekiti wa kitaifa wa Chama cha Wiper, Balozi Chirau Ali Mwakwere amesema kaunti za Pwani zitaimarika kiuchumi na maendeleo iwapo wananchi na viongozi watajitenga na siasa za ukabila, kidini na migawanyiko ya kisiasa.
Balozi Mwakwere ameshikilia kuwa changamoto zinazoshuhudiwa katika ukanda wa Pwani zimechangiwa na siasa potovu, akiwahishi wananchi wa Pwani kushirikiana ili kubadilisha hali hiyo.
Hata hivyo Chama cha Wiper kimemuidhinisha Sheikh Mahmoud Abdulrahman kuwa mgombea wa kiti cha uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Msambweni.