Story by Our Correspondents
Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amemteua Andrew Sunkuli kuwa mgombea mwenza wake.
Akizungumza katika halfa iliyoandaliwa jijini Nairobi, Kalonzo amemtaja Sunkuli kama kiongozi mwenye weledi katika ulingo wa siasa licha ya kuwa na taalum ya ualimu.
Kalonzo amewataka wakenya kuunga mkono azma yake ya kuwania kiti cha urais, akisema ushirikiano wake na Sunkuli atabadilisha maendeleo ya taifa hili sawa na kupambana na kashfu zote za ufisadi nchini.
Kwa upande wake mgombea mwenza wa Kalonzo, ambaye ni Sunkuli ameahidi kuhakikisha kampeni za kumpigia debe Kalonzo kuingia Ikulu zinafanikuwa huku akiwataka wananchi kuunga mkono azma hiyo kwani ndio itaunda serikali.
Hata hivyo halfa hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwemo Mwenyekiti wa kitaifa wa chama cha WIPER Balozi Chirau Ali Mwakwere, Mwenyekiti wa chama cha KANU Gideon Moi miongoni mwa viongozi wengine.