Picha kwa hisani
Kinara wa Chama cha WIPER Kalonzo Musyoka, amejitokeza na kupinga vikali kuhusika na sakata ya unyakuzi wa ardhi ya Yatta, akisema madai anayoelekezewa ni njama ya kuharibu sifa.
Kalonzo amepinga vikali madai, akisema wanyakuzi wakuu wa ardhi nchini wanajulikana lakini chakusangaza serikali imekosa kuwatia nguvuni.
Kiongozi huyo amewataka maafisa wa idara ya upelelezi wa jinai nchini kuingilia kati na kuchunguza madai hayo, akisema kamwe hajawahi husika na sakata za unyakuzi wa ardhi, huku akiitaka Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC kuchunguza mali zake zote.
Wakati uo huo amemkosa Naibu Rais Dkt William Ruto kwa kuchochea madai hayo wakati wa mikutano yake ya kisiasa katika kaunti ya Bomet, akisema viongozi kama Ruto wamepoteza muelekeo na kutafuta mbinu za kuwagawanya wakenya.