Picha kwa hisani –
Kinara wa chama cha WIPER Stephen Kalonzo Musyoka amefika mbele ya maafisa wa idara ya upelelezi DCI kuwasilisha stakabadhi zinazoonyesha uhalali wa umiliki wa ardhi yake ilioko katika eneo la Yatta.
Kalonzo amewasilisha stakabahi za ardhi hio ili kuchunguzwa uhalali wake,kwa lengo la kusafisha madai yalioibuliwa na naibu wa rais William Ruto kwamba alinyakua ardhi hio iliyoko chini ya shirika la vijana la NYS.
Mawakili wa Kalonzo wakiongozwa na seneta James Orengo wamemtaka Ruto kukoma kutoa matamshi ya uongo na uchochezi dhidi ya wanasiasa wenza,na badala yake kuzingatia sheria za nchi sawa na maadili ya cheo chake.
Haya yanajiri baada ya Naibu wa rais William Ruto akiwa kwenye mkutano eneo la Bomet siku chache zilizopita kudai kwamba Kalonzo alinyakua ardhi anayomiliki eneo la Yatta
Hata hivyo madai hayo yaliopingwa vikali na aliyekua waziri wa ardhi nchini gavana wa kitui Charity Ngilu aliyesema ana udhibitisho kwamba kiongozi huyo wa WIPER anamiliki ardhi hio kwa njia halali.