Story by Janet Shume
Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amefika mbele ya kamati ya watu Saba inayowapiga msasa waliotuma maombi ya wakenya wanaomezea mate nafasi ya kuwa mgombea Raila Odinga.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kikao hicho katika hoteli moja jijini Nairobi, Kalonzo amesema hajashurutishwa na mtu yeyote kufika mbele ya kamati hiyo kuhojiwa licha ya kuwa na tashwishi na kamati hiyo hapo awali.
Kalonzo amewahakikishia wakenya kwamba ana tajriba na uzoefu wa kutosha wa kumuwezesha kuwa naibu rais na kuleta mabadiliko nchini.