Picha kwa hisani –
Waziri wa Elimu nchini Profesa George Magoha amesema kalenda mpya ya masomo ya wanafunzi wote itatolewa hivi karibuni ili kuhakikisha wanafunzi hawapotezi mwaka mwengine wa masomo kufuatia changamoto za janga la Corona.
Akizungumza na Wanahabari katika kaunti ya Murang’a baada ya kufanya ukaguzi wa madawati, Magoha amesema tarehe ya mitihani kwa wanafunzi hao itaandaliwa kisha kutolewa kwa umma kwani shule hizo zitafunguliwa rasmi Januari mwakani.
Waziri Magoha amewahimiza wadau mbalimbali wa sekta ya elimu kushirikiana na wasimamizi wa shule ili kuhakikisha sheria za kudhibiti msambao wa virusi vya Corona zinatekelezwa kikamilifu.
Wakati uo huo amedai kuwa kufikia siku ya Ijumaa wiki ijayo madawati yote yalionunuliwa na serikali yatasambazwa shuleni kwani mradi huo unaigarimu serikali shilingi bilioni 1.9