Mchekeshaji Kura Tsuma maarufu kama Kalambua amempoteza mamake mzazi.
Taarifa kutoka kwa mcheshi huyo ambaye ni mfanyikazi wa Radio Kaya ni kuwa mamake mzazi aliaga dunia usiku wa tarehe 14 Januari baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Mazishi ya mwenda zake yatafanyika leo saa saba mchana kwao nyumbani Mwalaphamba, kaunti ya Kwale.
Radio Kaya inampa pole Kalambua na kumtakia nguvu wakati huu mgumu.
Taarifa na radio Kaya.