Story by our Correspondent –
Wizara ya Afya nchini imefanya kikao cha mazungumza na viongozi wa vyama vya kutetea maslahi ya walimu nchini ikiwemo Chama cha KNUT.
Katika kikao hicho kilichoandaliwa katika majengo ya Afya House jijini Nairobi, Waziri wa Afya nchini Mutahi Kagwe amesema Wizara hiyo imeandaa mikakati mwafaka ya kuhakikisha afya ya wanafunzi inalindwa shuleni.
Waziri Kagwe amesema swala la afya bora kwa wanafunzi, usafi na lishe na mazingira bora ya shule pia yamejadiliwa katika sera ya afya ya shule za Kenya iliyoanzishwa mwaka wa 2018.
Kwa upande wake Katibu mkuu wa chama cha KNUT Collins Oyuu ameipongeza Wizara ya Afya nchini kwa kuhakikisha walimu wanapata chanjo ya Corona huku viongozi hao wakiahidi kutumia matawi yao 110 kuwahimiza walimu kuchanjwa.