Picha kwa hisani –
Wakenya watabaka mbalimbali wamehimizwa kuendelea kuliombea taifa hili ili lizidi kuwa taifa la amani na uzalendo.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini Kadinali John Njue amesema huu ndio wakati wa viongozi kubadili mienendo yao na kushirikiana na wakenya katika kutumikia taifa .
Akizungumza wakati wa ibada ya Misa ya Jumapili ya kuombea Mitume katika Kanisa Katoliki la Holy Family Basilica jijini Nairobi, Kadinali Njue amesema uongozi hutoka kwa Mungu hivyo basi viongozi walio mamlakani hawafai kuliongoza taifa kwa mambo yao binafsi.
Wakati uo huo amewahimiza waumini wa Kanisa Katoliki kuendelea kuwa watumishi wema kwa kutekeleza yale yanayoendana na mafunzo ya mwenyeziMungu.