Kadhi mkuu nchini Sheikh Ahmed Muhdhar amewasihi wafuasi wa dini hiyo kuzingatia kikamilifu masharti ya kudhibiti Corona.
Sheikh Muhdhar amesema sawia na hali ilivyokuwa mwaka uliyopita, Ramadhan ya mwaka huu inakabiliwa na changamoto na ni sharti jamii hiyo ijikinge.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa, Sheikh Mudhar ameyataka makampuni yanayotoa huduma msingi kwa wananchi ikiwemo kampuni ya Kenya Power kuwajibika wakati wowote ule.
Wakati uo huo, amewarai wafuasi wa dini hiyo na wahisani wengine kuzidi kuzisaidia familia zisizojiweza wakati huu wa Mwezi mtukufu wa Ramadhan sawia na siku nyinginezo akihoji kuwa wakaazi wengi wa Pwani wanapitia hali ngumu.