Picha Kwa Hisani – Kabi Wa Jesus Instagram page
Familia ya wanamitandao maarufu “Wa Jesus” imeonyesha kutotikiswa na misukosuko wanayopitia. Milly wa Jesus ambaye ni mke wa Kabi Wa Jesus, amesema anaumia baada ya kugundua kuwa mumewe alidanganya kuhusu kuwa na mtoto nje ya ndoa lakini itabidi azoee.
Kabi wa Jesus hatimaye alikiri kuwa ana mtoto nje kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuomba msamaha kwa kujaribu kuwapotosha Wakenya wakati ripoti ziliibuka kuwa anawika mitandaoni ilhali mwanawe anahangaika.
Tetesi za Kabi kuwa na mtoto nje ya ndoa zilianza mapema mwaka jana lakini akapuuza akisema kipusa aliyekuwa akitajwa kuwa na mtoto naye alikuwa ni binamu yake.
Hata hivyo, ukweli sasa umethihirika baada yake kufanyiwa uchunguzi wa DNA ambao umedhibitisha kuwa alimzaa mtoto huyo wa kike kwa jina Abby.
Aidha, alisema atamfikia mama wa mtoto huyo mara moja ili aanza kutekeleza majukumu yake kama baba Abby.