Gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Jeffah Kingi amesema kuwa Jumuiya ya kaunti za Pwani imeweka mikakati thabiti kurudisha hadhi ya kitalii katika ukanda huu.
Kulingana na gavana Kingi, viongozi katika jumuiya hiyo watashirikiana na wadau wa sekta ya utalii kuboresha vivutio vya kitalii vinavyopatikana katika ukanda huu ili kuvutia watalii zaidi.
Kingi ametaja kuwa utalii ndio uti wa mgongo wa uchumi wa ukanda wa Pwani na kuna haja kuuboresha zaidi.
Tayari jumuiya hiyo ya kaunti za Pwani imejadiliana na serikali ya kitaifa kuhusu kuimarishwa kwa sekta ya utalii pwani na kuongeza idadi ya watalii hasa msimu huu wa likizo.
Taarifa na Esther Mwagandi.