Picha kwa hisani –
Gavana wa kaunti ya Taita taveta Granton Samboja, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa jumuiya ya kaunti za Pwani.
Akizungumza kwenye kikao kilicholeta pamoja magavana wa kaunti za pwani, Samboja amesema jumuiya ya kaunti za pwani inalenga kupigania maslahi ya wakaazi wa pwani.
Mwenyekiti huyo wa jumuiya ya kaunti za pwani amesema magavana wa kaunti za Pwani wameungana kuhakikisha eneo la Pwani linatambulika katika ngazi ya kitaifa.
Magavana wa kaunti za Pwani waliohudhuria kikao hicho kilichoandaliwa kaunti ya taita taveta ni Pamoja na Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho, Gavana wa Dhadho Godhana wa Tanariver, Gavana wa Lamu Fahim Twaha,na Amason Kingi wa Kilifi.