Picha kwa hisani.
Mwanamziki Julius Owino almaarufu Juliani ameandikisha taarifa kwa polisi akidai kwamba maisha yake yamo hatarini.
Haya yanajiri masaa machache baada yake kujitokeza na kuzungumza kuhusu madai kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na aliyekuwa mke wa gavana wa Machakos Alfred Mutua, Bi Lilian Ng’ang’a,
Mwanamuziki huyo anayefahaamika zaidi kutokana na nyimbo zake “Niko njaa” na “Utawala” alisema amekuwa akipokea jumbe za simu na kuonywa kwa kile alisema ni madai ya ‘kumuiba’ Lilian Ng’ang’a.
“Unaweza aje “iba mtu”?! Mtu mwerevu aliye na akili zake timamu?” aliandika kwenye twitter kuhusu madai hayo.
Juliani amekuwa akigonga vichwa vya habari tangu picha zake na Lilian zianze kuibuka kwenye mitandao.
Picha hizo zilianza kuibuka baada ya Lilian kutangaza kuwa ameamua kauchana na Gavana wa Machakos Alfred Mutua.
Wawili hao wamekuwa kwenye uhusiano kwa kipindi cha miaka 10 katika ndoa ambayo ilijaa mahaba kama ilivyoonekana mtandaoni.