Picha kwa hisani –
Waziri wa Utalii nchini Najib Balala, amesema juhudi za kuuzima moto unaoendelea kuteketeza mbuga ya kitaifa wa Tsavo bado zinaendelea na matumaini ya kuuokoa msitu huo zingalipo.
Waziri Balala, amesema tayari wadau mbalimbali wamejitolea kuisaidia Wizari hayo kuudhibiti moto huo sawia na kuwaokoa wanyamapori wanahifadhiwa katika mbuga hiyo.
Aidha amedokeza kuwa japo moto huo umeteketeza sehemu kubwa ya mbuga hiyo, ndege za shirika la huduma kwa wanyamapori nchini KWS zimesaidia pakubwa kuudhibiti moto huo kwa kiasi kikubwa.
Wakati uo huo amewataka watu wanaotembea karibu na mbuga za wanyamapori ama misitu kutochama taka hovyo kwani huenda tabia hiyo ikachangaia hatari zaidi.