Jopo la Makamishna 9 wa Tume ya huduma za mahakamani nchini JSC limempendekeza Jaji wa Mahakama ya rufaa William Ouko Okelo kuwa Jaji wa Mahakama ya Upeo.
Mwenyekiti wa jopo la JSC Profesa Olive Mugenda amesema zoezi la kuwapiga msasa watu waliotuma maombi ya kujaza nafasi ya Jaji wa Mahakama ya Upeo ilioachwa wazi baada ya kustaafu wa Jaji Jackton Ojwang lilitekelezwa kwa uwazi.
Profesa Mugenda amesema tayari jina la Jaji Ouko limewasishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta kufanya uteuzi wa nafasi hiyo sawia na kuliwasilisha katika bunge la kitaifa kupigwa msasa.
Iwapo Jaji Ouko ataidhinishwa rasmi na Rais Kenyatta sawia na bunge la kitaifa kuridhia uteuzi huo basi moja kwa moja ataapishwa rasmi na kuwa Jaji wa Mahakama ya upeo nchini.