Picha kwa hisani –
Jopo la makamishna tisa wa tume ya huduma za mahakama nchini JSC limeanza rasmi zoezi la kuwapiga msasa watu 10 walioorodheshwa kuwania nafasi ya jaji mkuu nchini iliyoachwa wazi na jaji David Maraga.
Tayari jaji wa mahakama kuu Said Juma Chitembwe ambae ameorodheshwa kuwa wa kwanza kuhojiwa amefika mbele ya jopo hilo kuhojiwa ambapo amepewa masaa manne kujieleza kuhusu uwezo wake wa kushikilia nafasi hio.
Akijitetea mbele ya Jopo hilo Chitembwe amesema kutokana na uzoefu wake wa kuhudumu kama jaji wa mahakama kuu nchini kwa zaidi ya miaka 12, atafanikisha mabadiliko makubwa katika idara ya mahakama nchini ikiwemo kumaliza mirundiko ya kesi mahakamani.
Chitembwe aidha amesema atakakikisha kesi zinazowasilishwa mahakamani zinasikizwa na kuamuliwa kwa muda mfupi ili kuhakikisha waliodhulumiwa wanapata haki kwa wakati.