Story by Bakari Ali –
Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho amewaonya wanasiasa dhidi ya kueneza siasa za chuki na migawanyiko miongoni mwa wananchi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wakaazi wa kaunti hiyo kuhusu umuhimu wa zoezi la usajili kama wapiga kura, Gavana Joho amesema ni sharti wanasiasa kuepuke siasa za uchochezi.
Joho amesema wakenya wanafaa kutambua umuhimu wa taifa la amani, huku akisema siasa za migawanyiko huenda zikaathiri pakubwa uchumi wa nchi.
Wakati uo huo, amewasisitiza wakaazi wa kaunti ya Mombasa kujitokeza kwa wengi na kujisajili kama wapiga kura ili wapate nafasi ya kuwachagua viongozi waadilifu.