Picha kwa hisani –
Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho amemsihi Rais Uhuru Kenyatta kuuongeza muda wa mradi wa Kazi mtaani ili kuwakimu vijana wanaokabiliwa na hali ngumu ya maisha.
Kulingana na Joho, mradi huo ni mwafaka na umewawezesha vijana wengi kunufaika.
Kwa upande wake, Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir amesema punde tu vyuo na taasisi zitakapofunguliwa vijana walionufaika na mradi huo watasajiliwa katika mradi wa Skills mtaani ili wapate taalama mbalimbali.