Zaidi ya wakaazi elfu 27 katika kaunti ya Mombasa wamepewa chanjo ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona.
Kulingana na Gavana wa kaunti hiyo Ali Hassan Joho, kaunti ya Mombasa ilipokea jumla ya chanjo elfu 30 na wameangazia wahudumu wa afya, Walimu, Maafisa wa polisi na hata wahudumu katika sekta ya utalii katika kaunti hiyo.
Akiwahutubia wanahabari alipoandamana na Mwenyekiti wa baraza la magavana nchini Martin Wambora, Joho amesema japo changamoto imekuwa hamasa kwa wakaazi wa kaunti hiyo, idara ya afya imewekeza zaidi katika kuwaelimisha wakaazi.
Joho amesema Serikali ya kaunti ya Mombasa imeweka mikakati muafaka ili kuchukua hatua za dharura endapo maambukizi yataongezeka katika kaunti hiyo.Mombasa