Picha kwa hisani –
Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho amemkosoa vikali Naibu Rais Dkt William Ruto, akisema Ruto hana ajenda ya maendeleo kwa wakenya.
Joho amesema Wakenya hawafai kumuunga mkono katika hazma yake ya kuwania urais wa mwaka wa 2022, huku akidai kuwa kiongozi huyo hafai kuwania kiti hicho.
Joho aliyekuwa akizungumza kule Mombasa, amezitaja siasa zinazoendelezwa na Ruto zilizobandikwa Jina la ‘Hustler nation’ kama zinazochangia umaskini badala ya kumuinua mkenya kimaisha.
Wakati uo huo, Joho amesema Ruto ana uwezo wa kuidhinisha miradi mbalimbali ya kuwakimu wakenya na hasa vijana kwa ajira akiwa bado ni Naibu Rais na wala sio hadi awa rais wa taifa hili.