John Elijah Mutunga kutoka shule ya msingi ya Masimbani kule Lungalunga kaunti ya Kwale ndiye mwanafunzi bora kaunti ya Kwale katika shule za msingi za uma katika matokeo ya mtihani wa darasa la nane ya KCPE yaliotolewa Ramsi na Waziri Wa Elimu Nchini George Magoha.
Mutunga alijizolea alama 417 kati ya alama 500.
Akizungumza na kituo hiki Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi ya Masimbani John Mutua amesema kuwa jumla ya watahiniwa 30 walifana katika mtihani huo Shuleni humo huku wa mwisho akajizolea alama 319.
Itakumbwa kuwa shule ya msingi ya Masimbani iliibuka Nambari Moja katika matokea ya mitihani Ya KCPE mwaka 2018 katika Ukanda wa Pwani kwa Shule Za Msingi Za uma na ya Pili kwa Shule zote za Kibinafsi na uma za msingi.
Juhudi za pamoja baina ya wazazi ,walimu na wanafunzi zimetajwa kama chanzo cha matokeo bora.