Picha Kwa Hisani
Mcheza santuri DJ Joe Mfalme amechapisha picha ya nyumba aliomjengea mama yake na kuambatanisha na ujumbe wa furaha kwa kutimiza mojawapo ya ndoto zake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Joe amewahakiki waliomtilia shaka na kumcheka miaka kumi na miwili iliyopita alipoamua kujitosa kwenye sekta ya usanii wa kucheza santuri yaani DJ.
“Wengi kule kijijini walinicheka na kujaribu kunikatisha tamaa huku wakiambia wazazi wangu kuwa kijana yao ameamua kuwa mkora” aliandika Joe.
Mashabiki wake walionekana kutiwa moyo baada ya DJ Joe kueleza kuwa kazi yake ya kucheza santuri ndiyo imemwezesha kununua shamba na kumjengea mama yake nyumba.
“Hii dunia usidharau kazi ya mtu. Nimesoma kuwa chochote unachoamua kufanya, tia bidii na uwe na nidhamu na utafanikiwa kwa neema zake Mola,” DJ huyo aliyepoteza kazi yake redioni Homeboyz baada ya madai uchochezi dhidi ya wanadada kwenye show yao kumkumba” aliandika Joe.
Picha Kwa Hisani
Hata hivyo wanamitandao wamempongeza kwa kukamilisha jengo hilo.