Picha kwa hisani –
Mitandao ya kijamii imewaka moto baada ya mwanamuziki Nameless kupokea kejeli nyingi alipofichua kuwa amekuwa akilala kwa kiti ili kuinusuru ndoa yake na msanii mwenzake Wahu ambaye ndio mke wake.
Hii ni baada yake kuwashauri wanaume wanunue viti na fanicha nzuri, kwa maana mambo uharibika katika vyumba vya kulala. Msanii huyo alipost ushauri wake kwa wanaume, kwa kweli hamna ndoa kamilifu, na wapiganao kwa hakika ndio wapendanao.
“Wanaume mimi huwaambia ukiweza, nunua sofa inaweza kuwa kitanda safi na TV clear ya kucheki movie. utakuwa tuu sawa kwa hii maneno ya ndoa sleeping on the couch ni kawa… make it comfortable.” – Nameless aliandika.
Nameless ambaye amekuwa kwa ndoa kwa muda wa miaka 15, na mkewe Wahu wamebarikiwa na watoto wawili huku akisema kuwa ndoa si kitanda cha maua wala mahala pa kujivinjari.
“Wacha niambie watu ukweli kuna nyakati ambazo nimelala kwa kiti, na ilisaidia ndoa yangu.” – Nameless aliandika.
Kauli yake ilizua hisia tofauti baina ya mashabiki wake, wengine wakikubaliana naye na wengine waki onyesha kushangaza na tabia za mke wake.