Picha Kwa Hisani –
Mwanamuziki wa bongo fleva Harmonize, amefunguka kuhusu mahusiano yake ya zamani na aliyekuwa mpenzi wake Jackline Wolper na kufichua sababu ya kuvunja uhusiano huo, jambo ambalo wengi hawakulifahamu.
Wikendi iliyopita, Harmonize ambaye pia anatambulika kama Konde boy au tembo alifichua kuwa Wolper alikuwa mdanganyifu na alitamani kuwa kwenye uhusiano na aliyekuwa bosi wake, mwanamuziki nyota wa bongo fleve, Diamond Platnumz.
Ufichuzi huu unajiri siku chache baada ya Wolper kusema kuwaHarmonize alimuacha baada ya kupata mpenzi mwingine, Sarah, ambaye sasa hivi ni mke wake. Madai ambayo Harmonize alipinga vikali katika hafla moja mjini Dodoma.
“Sio vizuri kuwasema wanawake lakini inaniumiza maana nliamua kukaa kimya lakini the more anafanya interviews, anasema mimi nlipata mzungu, sponsor nikamuaacha. Ki ukweli inaniuma sana… Kilichotufanya tuachane nina imani hata yeye hajui
…ilikuwa ni mwezi wa kwanza, tulikuwa na party nyumbani kwa kaka yangu, boss wangu wa zamani Diamond Platnumz. Tukawa tuna party, bila haya bila aibu, akawa anamtaka Diamond kimapenzi
Speaking from my heart, sijawahi kusema popote pale, leo ndio nasema ili ajue na mwenye kujua kama mimi najua. Akawa anamwambia Diamond kuwa atamzalia mtoto wa kiume, kipindi hicho Diamond ana mtoto mmoja tu Tiffa ambaye birthday yake ilikuwa jana maskini wa Mungu
Akamwambia atamzalia mtoto wa kiume, akamwambia hadhi yangu sio ya kutembea na Harmonize ili nipate ukaribu na wewe, I love you so much.” – Harmonize
Harmonize alisema kuwa licha ya kumpenda kwa dhati na kumzawadi gari la milioni 30 pesa taslimu za Tanzania, Wolperalikuwa mdanganyifu katika uhusiano wao na mara kadhaa alimpata na jumbe za kimapenzi za wanaume wengine.
Je, unazungumziaje swala hili?