Wananchi wametahadharishwa dhidi ya walaghai wanaojifanya kuwa na uwezo wa kuwasajili vijana katika kikosi cha jeshi nchini KDF, katika shughuli ya kusajili makurutu inayoendelea sehemu tofauti nchini.
Afisa anayesimamia zoezi la kusajili makurutu ka kaunti ya Kwale Luteni Kanali Joseph Nzioka ameeleza kuwa mara nyingi zoezi hili linapoendelea walaghai huwahadaa vijana na kuwapora fedha zao.
Nzioka amewaomba vijana kuwa waangalifu zaidi, akisema wale waliofuzu wanafaa kusubiri barua kutoka kwa serikali za usajili lakini sio kwa watu binafs.
Jumla ya vijana 5 kutoka gatuzi dogo la Matuga kaunti ya Kwale, wamefuzu kujiunga na kikosi cha jeshi katika zoezi la usajili wa makuruutu liliofanyika katika bustani ya uhuru garden mjini Kwale.
Taarifa na Mariam Gao