Picha kwa hisani –
Mwanamuziki na mfanyabiashara Faustina Charles almaarufu Nandy, amefunguka kuhusu tetesi za kunasa uja uzito wa mpenzi wake Bilnass. Nandy ameweka wazi kuwa hana ujauzito ila mwili wake umeongezeka kwa sababu ya mabadiliko ya binadamu.
Mwanamuziki huyo amesema mashabiki wameanza kumnyooshea vidole kuwa tayari amanasa ujauzito wa mchumba wake, Billnas jambo ambao sio kweli.
Baada ya kumvisha Nandy pete ya uchumba miezi michache iliyopita, Bilnas alifichua kutoshiriki mapenzi naye hadi wafunge ndoa.
“Watu wanasema mimi ni mjamzito kwa sababu nimenenepa, ukiangalia familia yetu wote wana maumbo makubwa halafu ni wanene labda na mimi ndio nimefikia hatua ya kuwa hivyo, sina mimba,” alisema Nandy.