Story by Ephie Harusi-
Serikali ya kaunti ya Kilifi imezindua rasmi majengo mapya ya kisasa ya kupeana huduma za upasuaji wa dharura kwa wananchi katika hospitali kuu ya kaunti ya Kilifi.
Kulingana na Gavana wa kaunti hiyo Amason Jefwa Kingi, wakaazi wa kaunti ya Kilifi hawatahitajika kusafiri hadi maeneo mengine kupokea matibabu ikiwemo hospitali kuu kanda ya Pwani iliyoko mjini Mombasa bali watapata huduma zote katika hospitali hiyo ya Kilifi.
Naye Waziri wa Afya kaunti ya Kilifi Charles Dadu amesema jengo hilo limeigharimu serikali ya kaunti ya Kilifi takriban milioni 800 kando na milioni 700 zilizotumika katika kununua vifaa mbali mbali vya matibabu.
Kwa upande wake Mzee wa mtaa wa eneo la Old Ferry Mkoka Kalume amewataka wauguzi katika hospitali ya Kilifi kuwajibikia majukumu yao jinsi inavyohitajika kwa wananchi.