Producer J Crack wa Crack sounds records kutoka kaunti ya Kilifi, mkoani Pwani amefananisha studio yake na Wasafi Classic Beiby (WCB) kutoka nchini Tanzania inayo aminika kumilikiwa na mwanamuziki nyota wa bongo Flavaz, Diamond Platnumz. Kupitia mahojiano na kikosi cha Kaya Flavaz kwa njia ya simu, J Crack alisema kwamba, kama tu WCB, Crack sounds pia imetoa wasanii wenye kazi nzuri na wanaotambulika kwenye kiwanda cha muziki. Aliongeza pia kwa kusema kuwa hata baada ya wanamuzikii hao kutoka kwenye recording label hiyo, bado analeta wengine ambao pia ni wazuri na kazi zao zinakubalika mkoani na hata nchini.
J Crack alitoa mfano wa rapper Mchafuzi wa mapozi alipotoka kukawa na Mtaliano Eliano, alafu Shabiggy, Susumila kisha kaa la moto ambapo wote, kazi zao zilifanya vyema mkoani hata kabla ya kutoka chini ya usimamizi wake, kwa recording label yake. Aliendelea kusema,hata baada ya wanamuziki hao kutoka, Crack sounds ikawaleta wasanii wengine ambao ni Medallion anayejulikana kwa wimbo wake maarufu ‘Kichuri’ na hivi majuzi ‘Ole Ole’ , Dhilly Dhilly kwa wimbo wake maarufu ‘Walk away’, Pat C Baba kwa wimbo wake maarufu ‘Gagada’ na pia Fikreen Mapito anayejulikana kwa wimbo wake ‘My Sugar’
Hii ni baada ya WCB kusign msanii wao wa kike wa pili hivi majuzi ambaye ni Zuchu na pia Mbosso baada ya kutoka kwa Harmonize na Rich Mavoko kwenye label hiyo. J Crack aliwapongeza wasimamizi wa WCB kwa kusign wanamuziki wapya bora zaidi kila mara mwingine anapotoka.
Producer huyo pia alifichua kufurahishwa na uwepo wa msanii ambaye pia ni Producer Dhilly Dhilly kwenye studio yake akimtaja kama mwenye bidii na kujituma na kusema kwamba anamuamini na kazi zake kwani alimfunza tangu akianza.
Je, maoni yako ni yapi kuhusu ufananisho wa recording label hizi?