Story by Our Correspondents-
Japhet Koome ameapishwa rasmi kuwa Inspekta jenerali mkuu wa Polisi nchini katika halfa iliyoandaliwa katika majengo ya Mahakama ya upeo.
Halfa hiyo iliyoongozwa na Jaji mkuu nchini Martha Koome imetekelezwa kwa kuzingatia sheria za nchi, huku akitarajiwa kulainishwa maswala tata nchini ikiwemo visa vya uvamizi wa mifugo na mauaji, sakata za ufisadi, sawa na kuimarisha usalama wa taifa.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kula kiapo cha kuhudumu katika afisi hiyo, Koome amewaonya vikali wahalifu akisema atakabiliana nao kikamilifu kwani wananchi wanahitaji usalama wa hali ya juu.
Kwa upande wake Jaji mkuu nchini Martha Koome amemsihi mkuu huyo wa polisi kuongoza idara hiyo kwa njia ya uwazi na uandilifu sawa na kufanikisha mageuzi bora katika idara ya polisi nchini.