Picha kwa Hisani
Bunge la kaunti ya Kilifi sasa linadai kuwa bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2020/2021 ya kaunti hio itaathirika pakubwa kutokana na janga la corona nchini.
Karani wa bunge hilo Micheal Ngala amefichua kuwa bajeti ya mwaka 2020-2021 itakua na mapungufu ya jumla ya shilingi bilioni 1.4 kutokana na athari za ugonjwa wa Corona.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya bajeti katika bunge la kaunti ya Kilifi Albert Kiraga amesema kaunti ya Kilifi itakumbwa na changamoto kutokana na kupungua kwa bajeti inayotokana na kupungua kwa mapato ya serikali ya kaunti hivi.
Kiraga anahoji kuwa janga la Corona limeathiri pakubwa ukusanyaji ushuru baada ya viwanda, timbo za mchanga sawa na mahoteli kufungwa kutokana na kusambaa kwa virusi vya Corona.