Shirika la Reachout Center Trust limeweka wazi kuwa visa vya waathiriwa wa dawa za kulevya kuhusishwa na uhalifu bado vinashuhudiwa katika kaunti ya Mombasa.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Taib Adhulrahman amesema hatua hiyo imetokana na waathiriwa wengi kununua dawa hizo kwa bei nafuu hasa mitaani na akapendekeza idara ya usalama kushirikiana na mashirika ya kijamii kupiga vita mihadarati.
Akizungumza mjini Mombasa, Taib amesema visa hivyo vitapungua endapo jamii itahamasishwa zaidi kuhusu jinsi ya kuishi na waathiriwa wa dawa za kulevya.
Wakati uo huo amefichua kuwa tayari Shirika hilo linashirikiana vyema na vyombo vya habari ili kuhakikisha vijana wanajinasua na utumizi wa dawa za kulevya.
Taarifa na Hussein Mdune.