Ni sharti jamii ya Ukanda wa Pwani ijizatiti katika kuwasaidia waraibu waliyojinasua katika utumizi wa dawa za kulevya kuregelea uraibu huo.
Mkuurgenzi mkuu wa Shirika linalopamba na uraibu wa dawa za kulevya Pwani la ‘Reachout Centre Trust’ Taib Abdulrahman amesema mara nyingi vijana wanaojinasua na kisha kuregelea tena uraibu wa dawa za kulevya huwa wamekosa ushauri wa mawazo na kuelekezwa jinsi watakavyodhibiti maisha yao upya.
Akizungumza mjini Mombasa hii leo, Taib amehoji kwamba ni lazima jukumu hilo litekelezwe kikamilifu na jamii yenyewe kabla ya vitengo mbalimbali vya Serikali kuingilia kati katika kuwasaidia Vijana hao kujitenga na uraibu wa dawa za kulevya.
Kulingana na Mwanaharakati huyo wa kupambana na uraibu wa dawa za kulevya Pwani, hata hivyo Serikali inapaswa kuidhinisha miradi mbalimbali kwa ajili ya kuwazuia vijana wanaojinasua kuregelea tena uraibu.