Story by Hussein Mdune-
Wadau wa sekta ya elimu katika kaunti ya Kwale wamedai kwamba kuna haja ya jamii katika kaunti hiyo kutilia maanani suala la elimu ya mtoto wa kike.
Wadau hao wakiongozwa na mchanganuzi wa masuala ya elimu katika kaunti ya Kwale Feisal Hassan, wamedai kwamba mtoto wa kike yuko na haki sawa na yule wa kiume hivyo basi anafaa kupewa elimu kwani ana uwezo mkubwa wa kuikabili jamii kimaendeleo.
Akizungumza na Wanahabari mjini Kwale, Feisal amewahimiza wazazi kuwapeleka watoto wao wa kike shuleni, akisema tabia ya taasubi ya kiume inafaa kukomeshwa katika jamii.
Feisal ambaye ni Mmiliki wa shule ya kibinafsi ya Mumtaz Academy ilioko mjini Kwale amesema ni kupitia elimu ndipo mtoto wa kike ataepukana na changamoto za maisha.